Washukiwa watatu zaidi wa wizi wa kimabavu wanaswa Kisumu

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa watatu zaidi wa wizi wa kimabavu wamenaswa mjini Kisumu na maafisa wa Polisi huku mali kadhaa za wizi zikipatikana.

Kunaswa kwa majambazi hao kunafuatia oparesheni nyingine iliyoendeshwa eneo la Nyawita kaunti ya Kisumu iliyosababisha kutiwa mbaroni kwa mshukiwa mkuu.

Mali kadhaa ya wizi ikiwemo runinga mbili mitambo miwili ya sauti, mitungi ya gesi ya kilo sita ,simu za rununu na panga mbili.

Aidha Polisi wamekamata pikipiki mbili za zinazofanyiwa uchunguzi huku msako wa washukiwa zaidi ukiendelea.

Washukiwa hao wanne watasalia korokoroni huku uchunguzi ukiendelea.

Share This Article