Saa chache baada ya kunasa bangi ya thamani ya shilingi milioni 35, polisi katika kaunti ya Marsabit wamewakamata washukiwa wanne wa ulanguzi wa bangi.
Wanne hao walikamatwa kwenye makutano ya Burgabo kwenye barabara ya Moyale-Marsabit.
Washukiwa walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota salon lenye nambari za usajili KDK 975B walipoamrishwa na polisi kusimama.
Baada ya upekuzi, polisi walipata vifurushi 12 vya bangi ndani ya buti ya gari hilo usiku wa kuamkia leo.
Inasemekana washukiwa walikuwa safarini kuelekea Marsabit wakitokea Moyale.
Wanne hao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Turbi na watafikiswhwa mahakamani Marsabit baadaye leo Ijumaa.