Washukiwa wanne wa ujambazi wakamatwa Kwale

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wa ujambazi wakamatwa Kwale.

Maafisa wa polisi wamewakamata washukiwa wanne wanaoaminika kuwa wanachama wa genge la ujamabazi eneo la Diani, kaunti ya Kwale.

Walikamatwa baada ya operesheni iliyotekelezwa na maafisa wa asasi mbali mbali za usalama, katika maeneo ya Magutu na Ukunda,kwenye kaunti ndogo ya Msambweni.

Washukiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha kadhaa zinazojumuisha mapanga na visu, kwenye operesheni hiyo ya alfajiri.

Kwa sasa wanazuiliwa kwenye korokoro za polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Huduma ya Taifa ya polisi (NPS), imetoa wito kwa umma kuwa waangalifu na kuendelea kutoa habari zitakazowasaidia maafisa wa usalama kukabiliana na uhalifu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article