Washukiwa wakuu 6 wa sakata ya uajiri wa wafanyakazi Nandi kushtakiwa

Martin Mwanje
1 Min Read
Stephen Sang - Gavana wa Nandi

Washukiwa wakuu 6 kwenye sakata ya uajiri wa wafanyakazi katika serikali ya kaunti ya Nandi wanatararjiwa kufikishwa katika mahakama ya Kapsabet baada ya kutiwa mbaroni jana Jumapili.

Washukiwa hao, akiwemo Afisa Mkuu wa kulipa mishahara na nduguye Gavana Sang, walikamatwa na maafisa wa ujasusi kwa madai ya kukosa kufuata sheria na utaratibu wa uajiri.

Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang bado anashikilia msimamo wake kuwa hatalegeza kamba kufuatia sakata hiyo.

Hii ni baada ya wakazi kuwasilisha malalamishi yao kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC mjini Eldoret wakitaka uchunguzi zaidi wa wafanyakazi waliopofutwa kazi.

Aidha, Gavana Sang aliyeonekana kuwa na ujasiri, amewaonya waathiriwa hao waliopigwa kalamu wasijaribu kutatiza na kulemaza shughuli zozote na operesheni katika idara mbalimbali za kaunti akisema watakabiliwa kisheria.

Share This Article