Katika juhusi za kushughulikia ongezeko la wizi wa kimabavu wa pikipiki na vifo vinavyotokana na hali hiyo katika eneo la Endebess na maeneo ya karibu, maafisa wa upelelezi kutoka makao makuu na wale wa kituo cha polisi cha Endebess walitekeleza oparesheni.
Oparesheni hiyo iliyokuwa ikongozwa na ujasusi waliokuwa wamepokea, ilisababisha kukamatwa kwa washukiwa wawili na kupatikana kwa pikipiki zinazoaminika kuibwa.
Sammy Mwangi Muriithi na Denis Wanjala Simiyu walikamatwa baada ya maafisa hao wa usalama kuvamia karakana yao kwa jina “Ex-Japan Spares” ambayo iko karibu na eneo la Veterinary la mji wa Kitale.
Ujasusi huo unaashiria kwamba baada ya kupokonya wamiliki pikipiki zao kimabavu na kuua wengine, pikipiki hizo huwasilishwa kwa karakana hiyo ambapo zinasambaratishwa na kuuziwa wateja wasiojua kama vipuri.
Wakati wa oparesheni hiyo, maafisa hao walipata pikipiki tatu, officers recovered three motorcycles, fremu tatu za pikipiki, nambari 26 za usajili wa pikipiki, sehemu mbali mbali za pikipiki na simu tatu za mkononi.
Washukiwa wanazuiliwa na maafisa wa polisi ambapo wanashughulikiwa wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku wamiliki wa pikipiki hizo wakitafutwa.