Washukiwa wa mauaji ya Richard Otieno wakamatwa

Martin Mwanje
1 Min Read
Washukiwa wa mauaji ya Richard Otieno ambao wamekamatwa na makachero wa DCI

Makachero wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI, wamewakamata washukiwa watano kuhusiana na mauaji ya Richard Haga Otieno yaliyotokea usiku wa Januari 18, 2025.

Washukiwa wakuu ni Geoffrey Mavado, John Ndegwa na Jorim Ngonga Sura wanaoshukiwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji hayo ya kikatili.

Washukiwa wengine wawili, Clinton Simantu almaarufu Muiruri na Peter Mwaniki almaarufu Pinchez ni wahudumu wa  bodaboda ambao wametambuliwa kama waliowasafirisha washukiwa kuelekea na kutoka eneo la mauaji.

Awali, Novemba 8, 2024, Mavado na Ndegwa walikamatwa na kushtakiwa kwa kumnyanyasa marehemu na kuhukumiwa kifungo cha uangalizi cha mwaka mmoja.

Washukiwa wote wanazuiliwa huku mipango ya kuwafungulia mashtaka mahakamani kuhusiana na mauaji hayo ikiendelea.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *