Washukiwa wa mauaji ya ajuza kaunti ya Vihiga wakamatwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Washukiwa wawili wa wizi wa kimabavu wanaoaminika kuwa sehemu ya genge lililomuibia, kumbaka na kumuua mwanamke wa umri wa miaka 76 mwezi uliopita  katika eneo la  Serem kaunti ya Vihiga, wametiwa nguvuni.

Washukiwa hao Patrick Misiko mwenye umri wa miaka 36 na Christine Jerono mwenye umri wa miaka 46, walikamatwa katika eneo la Majengo wakiwa na simu ya marehemu, ambayo ni sehemu ya mali iliyoibwa wakati wa uhalifu huo uliotekelezwa tarehe 18 mwezi Julai mwaka huu.

Usiku wa kisa hicho, majambazi hao walivunja nyumbani kwa ajuza huyo, huku wakimshambulia kwa silaha butu, na kisha kuendeleza unyama huo.

Washukiwa hao waliiba mitungi ya gesi, simu ya Mkononi na bidhaa zingine.

Majirani walimpeleka katika hospitali ya rufaa ya Mbale, lakini alifariki siku mbili baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata.

Maafisa wa polisi wanawahoji wawili hao, huku msako dhidi ya washirika wao ukiendelea.

TAGGED:
Share This Article