Washukiwa sita wa uhalifu wanaswa Kitale

Dismas Otuke
0 Min Read

Polisi wamewanasa vijana sita wanaoshukiwa kuhusika katika uhalifu katika mtaa wa mabanda wa Burma mjini Kitale.

Maafisa wa polisi walinasa vifaa vya kielektrioniki vinavyoaminika kuwa vya wizi, mali nyingine ya wizi, lita nne za pombe haramu ya chang’aa na silaha butu zinazokisiwa kutumika kwa shughuli za ujangili.

Washukiwa hao wawekwa rumande wakisubiri kufikishwa kortini.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article