Washukiwa 9 wa wizi wa simu wakamatwa Nakuru

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa 9 wa wizi wa simu wakamatwa Nakuru.

Maafisa wa polisi kaunti ya Nakuru wamewakamata washukiwa 9 wanaodaiwa kuhusika katika misururu ya wizi wa simu na pia uuzaji wa simu zilizoibwa.

Kulingana na taarifa ya Huduma ya Taifa ya Polisi, washukiwa hao walikamatwa baada ya operesheni ya kiusalama kutekelezwa katika maaeneo ya Shoppers Paradise na  Kaptembwa.

Kwenye operesheni hiyo, maafisa hao walipata simu kadhaa za rununu zinazoaminika kuwa za wizi na vipakatalishi vinavyodaiwa kutumiwa kuharibu nambari za siri za rununu hizo.

Wakati huo huo maafisa hao walipata vipande 16 vya bangi kwenye operesheni hiyo, huku huduma hiyo ya polisi ikielezea kujitolea kwake kuwalinda wananchi dhidi ya uhalifu.

“Huduma ya Taifa ya Polisi inajizatiti kukabiliana na uhalifu na kuhakikisha wanaojihusisha na aina yoyote ya uhalifu wanachukuliwa hatua za kisheria,” ilisema huduma hiyo kwenye taarifa.

Share This Article