Washukiwa 5 wakamatwa, lita 1,300 za pombe haramu zaharibiwa

Washukiwa hao wanazuiliwa kwenye korokoro za polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi waharibu lita 1,300 za pombe haramu Nairobi.

Maafisa wa Polisi wamewakamata washukiwa watano wanaodaiwa kuendesha biashara ya pombe haramu, huku lita 1,300 za pombe aina ya kang’ara zikiharibiwa katka mtaa wa Soweto Jijini Nairobi.

Washukiwa hao wanazuiliwa kwenye korokoro za polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Huduma hiyo ya Polisi imekariri kuwa haitalegeza kamba kwenye operesheni zake dhidi ya utayarishaji na usambazaji wa pombe haramu kote nchini Kenya.

“Vita dhidi yautayarishaji, usambazaji na utumizi wa pombe haramu, vitaendelea katika pembe zote za taifa hili,” Ilisema huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa X.

Aidha, kulingana na huduma hiyo, operesheni hizo zinalenga kulinda afya ya jamii na madhara mengine ya kiafya.

Share This Article