Washukiwa 5 wa wizi wa mabavu watoroka kizuizini Limuru

Watano hao walitoroka baada ya mlango wa chuma wa chumba walimokuwa kufunguliwa kwa lengo la kuwahamishia washukiwa 10 kwenye chumba kingine.

Martin Mwanje
1 Min Read

Washukiwa watano wa wizi wa mabavu wametoroka kizuizini katika kituo cha polisi cha Limuru huku juhudi za kuwasaka zikipamba moto.

Watano hao walitoroka baada ya mlango wa chuma wa chumba walimokuwa kufunguliwa kwa lengo la kuwahamishia washukiwa 10 kwenye chumba kingine.

Washukiwa watano waliotoroka ni Moses Waswa, Simon Eshiwani, Daniel Ndichu Njoroge, Dedan Kariuki na Edward Muriithi Kariuki.

Punde mlango ulipofunguliwa, washukiwa wanaripotiwa kuwakabili maafisa wa polisi waliokuwa kwenye zamu na kuwazidi nguvu na kisha kuchana mbuga.

Hii ilikuwa ni majira ya saa tano jana usiku.

Timu ya maafisa wa usalama ikiongozwa na Mary Njoki kwa sasa inaendeleza msako wa kuwasaka washukiwa hao.

Share This Article