Maafisa wa polisi wamewakamata washukiwa 39 zaidi, wanaoaminika kuwa wanachama wa magenge ya wahalifu katika kaunti ya kwale.
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema washukiwa hao walikamatwa baada ya operesheni iliyotekelezwa kwenye maficho yao kufuatia habari za kijasusi.
Washukiwa hao wa magenge ya uhalifu almaarufu ‘Panga Boys’ waliokamatwa leo Ijumaa ni pamoja na Ali Bakari Mwakuzimu, Hassan Ayub Cheti, Mohammed Salim Said, Mwalimu Rashid Mwakuzimu, Omar Abdurahman Mohammed, Shukran Seif Bengiji, Ibrahim William Okoyo, Matano Rashid Mwahambwe na Rashid Mwalimu Raso miongoni mwa wengine.
Operesheni hiyo ilitekelezwa katika maeneo ya Junda, Bilima, Barisheba, Sunlight, Mwandoni, Cobra, uwanja wa Kadongo, Mwakirunge na Vikwatani, authorities arrested 39 suspects linked to the machete-wielding gangs.
Kulingana na DCI, washukiwa hao pia walipatikana na silaha zinazoaminika kutumika katika shughuli zao za ujambazi, zinazojumuisha mapanga 11, visu vinne, pakiti 25 za bangi za bramu 50 kila moja, makasi, bastola bandia, pikipiki moja, msumeno na aina tofauti ya mavazi.
Washukiwa hao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mjambere na watachukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda wa polisi eneo la Pwani Ali Nuno, aliahidi kuanhgamiza makundi yote ya uhalifu katika eneo la pwani, ambayo yamewakosesha wakazi wa eneo hilo usingizi kwa muda mrefu.