Waziri wa Afya Aden Duale, ameagiza Halmashauri ya Kusambaza Dawa Nchini KEMSA , kuharakisha utekelezaji wa marekebisho kuambatana na ajenda ya afya ya serikali chini ya mpango wa Botto Up, na kufanikisha mpango wa Bima ya Afya kwa wote UHC.
Akiongea wakati wa mkutano wa mashauriano na bodi ya usimamizi ya KEMSA pamoja na maafisa wakuu wa halmashauri hiyo katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi, Duale alisisitiza umuhimu wa kurejesha imani ya wananchi kwenye shughuli ya kusambaza dawa, ambayo huanza na mageuzi ya kitaasisi, ufanisi na uongozi wenye maadili.
Duale alipongeza mabadiliko yanayotekelezwa na KEMSA na kuitaka halmashauri hiyo kuharakisha utekelezaji wa kanuni chini ya sheria inayosimamia halmashauri ya KEMSA.
Duale aliitaka KEMSA kudumisha umoja, uadilifu na uwajibikaji ili kufanikisha mpango wa afya kwa wote.
Duale alikuwa ameandamana na Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt. Patrick Amoth na viongozi wa KEMSA akiwemo Afisa Mkuu Mtendaji wa KEMSA Dkt. Ejersa Waqo.