Washukiwa 10 walinasawa siku ya Jumatano kwenye msako wa polisi ulioendeshwa kuwatafuta wahusika waliovamia nyumba moja na kuwaibia wenyeji, na kisha kuteketeza nyumba katika eneo la Mjambere, Kisauni katika kaunti ya Mombasa.
Maafisa wa polisi wanawasaka washukukiwa zaidi ambao ni sehemu ya genge ambalo limekuwa likiwahangaisha wananchi.
Awali, genge hilo lilivunja nyumba ya vyumba vinne ya kupangisha ya Uswahili wakiwa wamejihami kisha kupora pia duka moja na kuiba bidhaa.
Wakazi wamekuwa wakilalamikia kuongezeka kwa visa vya uhalifu katika eneo hilo na maeneo kama vile kijiji cha Toa Tugawe.