Washiriki zaidi ya 8,000 wajiandikisha kwa mbio za Nairobi City

Dismas Otuke
1 Min Read

Washiriki zaidi ya 8,000 wamejiandikisha kushiriki makala ya pili ya mbio za Nairobi City Marathon Jumapili hii, Julai 2.

Kulingana na mkurugenzi wa mbio hizo ambaye ni aliyekuwa bingwa mara tatu wa Boston Marathon Ibrahim Hussein, wamebadilisha mkondo wa mbio za mwaka huu za kilomita 42, zikianzia katika barabara ya Douglas Wakihuri badala ya barabara ya Langata ilivyokuwa mwaka jana.

Mbio za kilomita 21 na kilomita 10 zitakimbiwa kwenye barabara ya Express Way pekee huku kilomita 42 ikiwa na mseto wa Express Way na barabara za kupita katikati ya jiji.

Makala ya mwaka huu kufikia sasa yameshuhudia usajili wa wanariadha kutoka mataifa 28 ikiwemo Tanzania, Ethiopia na China huku washindi wa Marathon wakituzwa shilingi milioni 3 nukta 5, nambari 2 shilingi milioni 2 na robo huku mshindi wa nafasi ya tatu akitia kibindoni shilingi milioni 1 nukta 5 kwa wanaume na wanawake.

Rais wa Cchama cha Riadha Kenya Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei amesema kuwa wanapania kupanda miche 15,000 wakati wa mbio za Jumapili kama nji moja ya kuafikia ruwaza ya serikali ya kuwa na idadi toshelzi ya miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Website |  + posts
Share This Article