Washindi wa medali za Olimpiki watuzwa pesa

Dismas Otuke
1 Min Read

Washindi wa nishani za Olimpiki  wametuzwa pesa na serikali baada ya kulakiwa katika Ikulu ya Eldoret na Rais William Ruto siku ya Alhamisi.

Kila mshindi wa nishani ya dhahabu ametuzwa shilingi milioni 3, washindi wa nishani za fedha wakapokea shilingi milioni 2, na washindi wa medali za shaba watia kibindoni shilingi milioni 1 kila mmoja.

Wanariadha hao walioshiriki Olimpiki waliandaliwa dhifa na Rais Ruto kama njia ya kuwasherehekea mashujaa hao.

Kenya ilizoa medali 11 katika mashindano ya Olimpiki ikichukua nafasi ya 17 kwa jumla.

Share This Article