Wasanii wa Tanzania wamepanga hafla ya kuwakumbuka wasanii wenzao ambao wameshaaga dunia iliyopatowa jina la “Faraja ya Tasnia”.
Shughuli hiyo itawaleta pamoja wahusika mbali mbali wa Tasnia ya burudani nchini Tanzania Septemba 7 2024 katika uwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa waandalizi wa hafla hiyo ambaye ni mwigizaji Steve Nyerere alisema lengo lao ni kuwaenzi wenzao ambao walitumia vipaji vyao mbali mbali kugusa maisha ya wengi na kamwe hawasahauliki.
Wasanii hao wa Tanzania kwa umoja wao wamekaribisha umma kujiunga nao siku hiyo ambapo familia za wasanii hao walioaga pia zitakumbukwa na kusaidiwa ipasavyo.
Kulingana na mabango ya hafla hiyo watakaokumbukwa siku hiyo ni pamoja na mwigizaji Steve Kanumba, mchekeshaji Mzee Majuto, Mwimbaji Bi. Kidude kati ya wengine wengi.