Maafisa wa polisi huko Nevada nchini Amerika wamethibitisha kwamba walitoa kibali hivi maajuzi cha kufanya uchunguzi nyumbani kwa matehemu Tupac Shakur, kuhusiana na kesi ambayo bado haijaamuliwa ya mauaji yake mwaka 1996.
Maafisa wa upelelezi tayari wamefanya wamezuru makazi hayo ya Shakur katika eneo la Henderson huko Las Vegas huku wakitafuta ukweli kuhusu mauaji ya Shakur kwa kupigwa risasi miaka 27 iliyopita.
Maafisa wa polisi hawakutoa taarifa zaidi kuhusu uchunguzi huo. Shakur aliuawa akiwa na umri wa miaka 25.
Makazi ambayo maafisa wa polisi walizuru yako umbali wa kilomita yapata 32 kutoka eneo ambalo mwanamuziki huyo wa mtindo wa rap alipigwa risasi na watu waliokuwa kwenye gari lililokuwa likipita.
Afisa wa polisi katika eneo hilo la Las Vegas Jason Johansson aliambia wanahabari kwamba majasusi wanajaribu kwa mara nyingine kuamsha kesi hiyo. Alisema anatumai kwamba siku moja watafanikiwa kutatua kesi hiyo kikamilifu.
Shakur, alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 1991 na baadaye akawa anaafikia ufanisi kwenye ulingo wa muziki wa rap. Alikata roho Septemba 13, 1996, wiki moja baada ya kupigwa risasi mara nne akiwa kwenye gari lake mahali ambapo alikuwa amesimamishwa na taa za trafiki.