Jeshi la Israel limetoa makataa ya saa 24 kuanzia mapema leo Ijumaa kwa Wapalestina wote kuhama Gaza kabla ya kushambulia ukanda huo.
Watu milioni 1.1 wanalazimika kuhama kufikia Ijumaa usiku, kuepuka kuangamizwa na majeshi ya Israel ambayo yamekuwa yakishambulia eneo hilo kwa wiki moja sasa.
Tayari raia 423,000 wa Palestina wameachwa bila makao katika Ukanda wa Gaza tangu kaunza kwa mashambulizi hayo.
Mashirika ya haki za kibinadamu yanaonya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi endapo majeshi ya Israel yatatekeleza mashambulizi hayo baada ya kutoa onyo.