Wapalestina waanza kurejea Kaskazini mwa Gaza

Tom Mathinji
1 Min Read
Wapalestina waanza kurejea Gaza. Picha/AFP.

Saa kadhaa baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas kuafikiwa, Wapalestina waliokuwa wametoroka makawao sasa wameanza kurejea kaskazini mwa Gaza.

Wanajeshi wa Israel wameanza kuondoka Gaza,  huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimshukuru Rais Donald Trump wa Marekani, kwa kufanikisha makubaliano hayo.

Hata hivyo, vikosi vya ulinzi vya Israel (IDF), vimesema vitaendelea kuondoa vishio vyovyote.

Chini ya mkataba huo uliotangazwa kwa mara ya kwanza na Rais Trump juma lililopita na kutiwa saini baada ya mashauriano ya siku kadhaa nchini Misri, Israeli sasa ina saa 24 kuondoka hadi sehemu iliyokubaliwa kwenye himaya ya Palestina.

Hamas baadaye itakuwa na saa 72 kuwaachilia mateka wote wa Israeli wanaozuiliwa huko Gaza, huku Israeli ikiwaachilia mamia ya wafungwa wa Palestina.

Marekani itawapeleka wanajeshi 200 nchini Israel kusaidia kufanikisha mpango wa usitishaji vita, haya yamesemwa na maafisa wa Marekani.

Website |  + posts
Share This Article