Katika moyo wa kusherehekea siku kuu ya Krismasi Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi, ametoa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakongwe 300 kutoka eneo bunge lake.
Mbunge huyo alihimiza haja ya Wakenya kusherekea pamoja ma kuwakumbuka wasiobahatika katika jamii msimu huu wa shamrashamra za siku kuu, licha ya hali ngumu ya kiuchumi iliyotokana na mfumko wa bei za bidhaa.
Wakongwe hao waliowajuisha akina mama na wanaume walitoka katika wadi tano za eneo bunge hilo.
Wanyonyi amekuwa akitoa msaada kwa makundi mbalimbali ya watu wa Westlands mara kwa mara.