Mshindi wa nishani ya fedha dunia mwaka huu katika mbio za mita 800,Emmanuel Wanyonyi, ameteuliwa katika orodha ya mwisho ya wanariadha watatu wanaowania tuzo ya chipukizi bora wa mwaka ya shirikisho la Riadha Ulimwenguni.
Wanyonyi ametamba msimu huu akiibuka mshindi wa mbio za nyika duniani katika shindano la kupokezakana kijiti mseto,kabla ya kushinda mikondo mitatau ya Diamond League ,mashindano ya Rabat,Paris na Xiamen.
Wengine wanaowania tuzo hiyo ni Roshawn Clarke wa Jamaica, aliyemaliza wa nne katika mita 400 kuruka viunzi wakati wa mashindano ya dunia na Erriyon Knighton wa Marekani aliyeshinda medali ya fedha ya dunia katika mita 200.
Mshindi atatangazwa tarehe 11 mwezi ujao kwenye hafla itakayoandaliwa mjini Monaco Ufaransa.