Takriban Wapalestina 9,000 wamefariki tangu kuanza kwa vita katika ukanda wa Gaza, majeshi ya Israel yakipigana na wanamgambo wa kundi haramu la Hamas.
Kulingana na maafisa wa Gaza watu 195 wameuawa huku wengine 120 wakiwa hawajulikani waliko kufuatia shambulizi katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia .
Umoja wa mataifa unakisia kuwa zaidi ya watu 300,000 wameachwa bila makao kutokana na vita hivyo huku idadi nyingine ya watu milioni 2 nukta 3 ya wakazi wa Gaza, wakikosa bidhaa muhimu za matumizi.
Uturuki imetangaza nia ya kuwahudumia wagonjwa wa saratani wa Palestina, baada ya Hospitali ya Gaza waliyokuwa wakihudumiwa kufungwa kwa kukosa Dizeli.