Wanyonyi ana imani ya kushinda ugavana Nairobi mwaka 2027

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi ameelezea matumaini yake ya kunyakua kiti cha Ugavana wa kaunti ya Nairobi katika uchaguzi wa mwaka 2027 .

Wanyonyi amesema haya siku ya Jumapili katika kaunti ya Kakamega alipohudhuria maombi ya shukran katika kanisa la Shinyalu.

Mbunge huo ambaye ni wakili alijiondoa katika kinyangányiro kufuatia ushauri na viongozi wa chama cha ODM na mrengo wa Azimio na badala yake kuhifadhi kiti chake cha Westlands kwa muhula wa tatu.

Wanyonyi alikiri kuwa amejiandaa vyema kumbwaga gavana Johnstone Sakaja katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Mbunge huyo pia amekeriri umuhimu wa jamii ya Abaluhya kuwa na umoja na sauti.

Share This Article