Wandayi atetea nyongeza ya bei za mafuta

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi.

Ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, limesababishwa na vita vilivyoshuhudiwa kati ya Israel na Iran mwezi Juni. Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa kawi Opiyo Wandayi.

Akizungumza leo Alhamisi katika kaunti ndogo ya Kajiado ya Kati, kaunti ya Kajiado, wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji umeme na kawi safi katika maeneo ya mashinani utakaogharimu shilingi bilioni 1.3, Wandayi alisema taifa hili limeathirika pakubwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani, kuliko sababishwa na vita hivyo.

Matamshi ya Wandayi yanajiri siku chache baada ya Halmashauri ya kuthibiti bei ya Kawi na Mafuta (EPRA) , kuongeza bei za mafuta Julai 14,2025.

Kulingana na Wandayi, bei za mafuta hapa nchini ni nafuu zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine kanda ya Afrika Mashariki na Kati, akidokeza kuwa  bei hiyo imekuwa ikipungua hadi wakati ambapo mzozo wa kimataifa ulipozuka.

Mradi huo wa umeme ulizinduliwa katika vijiji vya Olchoro Onyori na Kimuka katika kaunti ya Kajiado .

Share This Article