Wanawake waandamanaji waliokuwa uchi nchini Uganda waachiliwa huru

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanawake watatu waliokamatwa wakishiriki maandamano ya kupinga serikali ya Rais Museveni wakiwa uchi mjini Kampala Uganda, wameachiliwa huru.

Hakimu wa mahakama ya Buganda Road amewaachilia huru wanawake hao watatu kwa dhamana siku ya Alhamisi.

Watatu hao Norah Kabusingye,Praise Aloikin na Kemitoma Kyenzibo waliachiliwa huru kwa dhamana ya mdhamini ya shilingi milioni moja za Uganda na Hakimu Ronald Kayiizi.

Watatu hao walikanusha kosa la kusabibisha kero na usumbufu kwa umma walipokuwa wakiandamana nje ya bunge la Uganda  Septemba 2 kupinga ufisadi serikalini.

Kabusingye ni mwanafunzi wa somo la biashara katika chuo kikuu cha Makerere huku Praise na Kyenzibo, wakisomea uanasheria pia katika chuo kikuu hicho cha Makerere

Share This Article