Wanawake wa sekta ya utalii wajiunga na KUDHEIHA kumaliza dhuluma za kijinsia

Aidha warsha hizo zitahimiza umuhimu wa kumaliza unyanyapaa kwa waathiriwa wa dhulma za jinsia na kimapenzi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Wafanyikazi wa Mikahawa, Taasisi za Elimu na Hospitali (KUDHEIHA), kimesaini mwafaka wa ushirikiano pamoja na chama cha wanawake katika sekta ya utalii nchini (KAWT) ili kukomesha dhuluma za kimapenzi na kijinsia dhidi ya wanawake kazini.

KAWT imeitaka serikali kutekeleza kikamilifu sheria za kumaliza visa vinavyoongozeka kila kuchao vya dhuluma za kimapenzi, kijinsia na mauaji ya wanawake.

Mwenyekiti wa KAWT Pauline Nduva amesema kuwa watashirikiana na KUDHEIHA katika kufanya uhamasisho dhidi ya dhuluma za kijinsia na kimapenzi kote nchini kupitia kwa warsha na mafunzo hususan kwa wanawake walio kwenye ajira.

Aidha, warsha hizo zitahimiza umuhimu wa kumaliza unyanyapaa kwa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia na kimapenzi.

Katibu Mkuu wa KUDHEIHA Albert Njeru ameitaka serikali kuwa katika mstari wa mbele kuteleza sheria za kuwaadhibu wale wanaotekeleza uovu huo.

Kulingana na takwimu, asilimia 34 ya wanawake humu nchini wameathiriwa na visa vya dhuluma za kimapenzi na kijinsia wakiwa na umri wa miaka 15 huku asilimia 13 ya wanawake wakidhulumiwa kimapnezi.

Leo Jumatano ni siku ya pili ya kipindi cha siku 16 za uanaharakati wa kupinga dhuluma za kijinsia na kimapenzi dhidi ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka kati ya Novemba 25 na Disemba 10.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *