Timu ya Kenya iliyonyakua ubingwa wa dunia katika mbio za nyika mjini Belgrade, Serbia ilirejea nchini siku ya Jumatatu.
Timu hiyo ilikaribishwa na maafisa wa chama cha Riadha Kenya.
Kenya ilihifadhi taji ya dunia Jumamosi iliyopita kwa kuzoa jumla ya medali 11, dhahabu 6, fedha 2 na shaba 3.
Matokeo hayo yalikuwa bora kuliko yale ya mwaka jana mjini Barthust nchini Australia, ilikonyakua dhahabu 6, fedha 2 na shaba 2.
Beatrice Chebet alihifadhi taji ya kilomita 10 huku akiwaongoza Wakenya kutwaa nafasi 5 za kwanza.