Wanariadha takriban 10,000 wajisajili kwa Chepsaita Cross Country

Dismas Otuke
2 Min Read

Takriban wanariadha 10,000 wamejiandikisha kushiriki  makala ya pili ya mbio za The Great Chepsaita Cross Country zilizoratibiwa kuandaliwa taehe 7 mwezi ujao katika kaunti ya Uasin Gishu.

Kulingana na waandalizi usajili katika vitengo vikuu tayari umefungwa huku washiriki wakiwa katika vitengo vya kilomita 10 wanaume na wanawake,kilomita 8 na 6 kwa chipukizi,mbio za wakongwe na mbio za kujiburudisha.

Kulingana na mwasisi wa mbio hizo Farouk Kibet,lengo lake ni kuhamasisha umuhimu wa kuwasomesha watoto ili wajumuishe talanta na masomo pamoja na kuleta maendeleo.

“Lengo kuu sio tu kukimbia bali kupanua miradi ya maendeleo na jamabo la pili ni kuinua talent ndio maana tunahimiza umuhimu wa kukimbia na kusoma,unyanyasaji mwingi unataoka kwa managers wa wanariadha kwa sababu ya kukosa masomo miaka inayokuja tuanataka tupate barabara ya lami kuunganisha kaunti nne”.akasema Kibet

Mkurugenzi wa mbio hizo ambazo zimepandishwa hadi hadhji ya dhahabu Barnaba Korir, amesema mbio hizo zitabadilisha eneo hilo la Chepsaita.

Mwenyekiti wa riadha kenya eneo la South Rift Abraham Mutai amesema matayarisho yamekamilika, huku wanariadha kutoka zaidi ya nchi 15  wakijiandikisha kushiriki.

Bingwa mara tanoi wa Dunia Geofrey Kamworor na mshindi wa dhahabu  mbili za Olimpiki Beatrice Chebet walihudhuria uzinduzi huo wa jana katika kaunti ya Uasin Gishu.

Washindi wa kilomita 10 kwa wanaume na pia wanawake watatuzwa shilingi 300,000.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *