Wanariadha kunufaika baada ya AK kupata ufadhili wa shilingi milioni 15 kutoka kwa Betika

Washindi wa kilomita katika mashindano ya mbio za nyika watatuzwa shilingi laki moja unusu ,washindi wa chipukizi chini ya miaka 20 shilingi laki moja na shilingi 50,000 kwa washindi wa kilomita 2 kupokezana kijiti.

Dismas Otuke
2 Min Read

Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya mbio za nchi na yale ya uwanjani wanatarajwia kunufaika pakubwa kufuatia kusainiwa kwa ufadhili wa kima cha shilingi milioni 15, kati ya chama cha riadha Kenya na kampuni ya kamari Betika kupitia kwa mradi wake wa Betika na Community.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Rais wa chama cha riadha Kenya, Jenerali mstaafu Jacksoin Tuwei, amesema ushirikiano huo unaojulikana kama Road to Tokyo utashuhudia shilingi milioni 5 zikilipwa kwa wanariadha watakaoshiriki mikondo mitatu iliyosalia ya mbio za nyika .

kiwango kingine cha milioni 10 kimetengewa mashindano ya raidha ya uwanjani ya Weekend Meet kuelekea hadi majaribio ya kitaifa kuteua kikosi cha Kenya kwa mashindano ya dunia mwaka ujao mjini Tokyo, Japan.

“Tumefurahia ushirikiano huu ambao unaashiria kujitolea kwa Kampuni ya Betika kuinua michezo nchini .Kile tunataka sasa ni kusaini mkataba wa muda mrefu utakajumuisha michezo ya Olimpiki mwaka 2028 nchini Marekani.”akasema Tuwei

Washindi wa kilomita katika mashindano ya mbio za nyika watatuzwa shilingi laki moja unusu ,washindi wa chipukizi chini ya miaka 20 shilingi laki moja na shilingi 50,000 kwa washindi wa kilomita 2 kupokezana kijiti.

Afisa mkuu mtendaji wa Betika Mutava Mutua amesema ana imani kuwa ushurikiano huo utabadilisha maisha ya wanariadha humu nchini.

“Ushirikiano wetu unaashiria kujitolea kwetu kunua riadha nchini.Riadha ni mchezo ambao umeiletea kesnya sifa nyingi kimataifa na tunajivunia kuchangia katika ukuzaji talanta.”akasema Mutua.

Riadha Kenya na kampuni ya Betika wameanza mkakati ya kusaini mkataba wa muda mrefu utakaogharamia matayarisho ya timu ya Kenya kwa michezo ya Olimpiki mwaka 2028 mjini Los Angeles, Marekani, ili kuhakikisha matokeo bora kuliko yale ya mwaka huu Jijini Paris.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *