Wanariadha 74 wateuliwa kuwakilisha Kenya, mashindano ya Afrika nchini Ghana mwezi ujao

Dismas Otuke
1 Min Read
SONY DSC

Wanariadha 74 wametajwa na chama cha Riadha Kenya kushiriki makala ya 24 ,ya mashindano ya bara Afrika mwezi ujao mjini Accra,Ghana.

Kikosi hicho kimetangazwa Jumamosi baada ya kukamilika kwa majaribio ya kitaifa ya siku tatu uwanjani Ulinzi.

Hata hivyo mabingwa wa Dunia na Olimpiki Na wanariadha wengine tajika wameachwa nje ya kikosi hicho wakiwemo Faith Kipyegon,Faith Cherotich na Emmanuel Wanyonyi.

Wanariadha wengi chipukizi wamepewa nafasi kwenye kikosi hicho .

Mashindano ya Afrika yataandaliwa nchini Ghana baina ya Mei 12 na 17 mwaka huu huku Kenya, ikilenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 ilipomaliza ya pili kwa dhahabu 9 fedha 5

na shaba 5 nyuma ya mabingwa Afrika Kusini.

Kikosi kamili kilichotajwa

 

Share This Article