Chama cha Riadha Kenya kimeteaua wanariadha 35 watakaoshiriki makala ya 31, ya michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa baina ya Julai 26 na Agosti 11 mwaka huu.
Timu hiyo inawajmuisha wanariadha chipukizi na wale waliobibea imechaguliwa Jumamosi, kufuatia kukamilika kwa majaribio ya kitaifa ya siku mbili.
Mshikili wa rekodi ya dunia ya mita 10,000 Beatrice Chebet na bingwa mara mbili wa Olimpiki Faith Kipyegon, watashiriki mashindano mawili kila mmoja.
Susan Ejore na Nelly Chepchirchir wataungana na Faith Kipyegon katika mita 1,500, huku timu ya wanaume ikimshirikisha bingwa wa zamani wa duna kwa chipukizi Raynold Kipkorir na bingwa wa dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot.
Bingwa wa dunia Mary Moraa atashiriki mita 400 pamoja na kujiunga na Lillian Odira kwenye mita 800.
Kikosi kilichotajwa ni kama kifuatavyo:
100m men
Ferdinand Omanyala
400m Women
Mary Moraa
400mH
Wiseman Were
800m women
Lillian Odira
Mary Moraa
800m Men
Emmanuel Wanyonyi
Wycliff Kinyamal
Koitatoi Kidali
1500m men
Raynold Kipkorir
Timothy Cheruiyot
1500 women
Faith Kipyegon
Nelly Chepchirchir
Susan Ejore
3000msc Women
Faith Cherotich
Jackline Chepkoech
Beatrice Chepkoech
3000msc men
Amos Serem
Simon Koech
Abraham Kibiwott
5000m women
Faith Kipyegon
Beatrice Chebet
5000m men
Ronald Kwemoi
Jacob Krop
Edwin Kurgat
10,000m women
Beatrice Chebet
Lillian Kasait
Margaret Chelimo
10,000m men
Daniel Mateiko
Nicholas Kipkorir
Bernard Kibet
Marathon Women
Peres Jepchirchir
Hellen Obiri
Brigid Kosgei
Sharon Lokedi-Reserve
Marathon men
Eilud Kipchoge
Alexander Mutiso
Benson Kipruto
Timothy Kiplangat-Reserve
Kikosi hicho kimeagizwa kuripoti kambini Jumanne ijayo kuanza mazoezi ya Olimpiki.