Wanamuziki kupokea malipo bora, asema Dkt. Ezekiel Mutua

Dismas Otuke
2 Min Read

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Haki za Wanamuziki Nchini, MCSK Dkt. EZekiel Mutua ametangaza kuwa wanalenga kukusanya shilingi bilioni nne ifikiapo mwezi Disemba mwaka huu. Amewahakikishia wanamuziki kuwa watapata malipo bora kuliko miaka ya nyuma.

Akizungumza na KBC kwa njia ya kipekee, Dkt. Mutua amesema malipo hayo ya juu yanatarajiwa baada ya Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kufanya kuwa sheria viwango sita vya ushuru unaotozwa watumiaji wa muziki.

“Hii ni habari njema, nimekuwa nikisukuma kuongezwa kwa matozo ya watumizi wa muziki, ukiangalia kila kitu kimepanda kuanzia kwa gharama maisha,” Mutua alisema.

Kufuatia kupitishwa kuwa  sheria kwa malipo mapya ya juu kwa wale wanaotumia muziki nchini, nina uhakika tutakusanya shilingi bilioni 4 ifikiapo Disemba na tutamwalika Rais atoe hundi hiyo kwa wanamuziki.”

Pia amevitaka vyama vinavyowasimamia wanamuziki maarufu kama CMOs kufanya kazi kwa pamoja na mashirika ya serikali ili kuhakikishwa wakiukaji wa haki wanaadhibiwa.

“MCSK kwa ushirikiano na wadau wake wanapanga kuzindua mfumo wa kidijitali ambao wanamuziki watatumia kufuatilia jinsi muziki wao unavyochezwa na kiwango cha malipo wanachostahiki kufikia mwezi Oktoba mwaka huu”

Kulingana na Dkt. Mutua, Kenya pia imesaini mikataba kadhaa na mataifa ya ughaibuni kuhakikisa wasanii wa humu nchini wanalipwa wakati miziki yao inapochezwa katika mataifa ya kigeni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *