Wanamichezo 81 wa Kenya watashiriki makala 33 ya michezo ya Olimpiki, itakayoandaliwa jijini Paris,Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11.
Kikosi hicho kitasaidiwa na jumla ya wakufunzi 43,maafisa watano wa kamati ya Olimpiki Kenya NOC-K,wasimamizi 26 na maafisa watatu watakaoongoza ujumbe huo.
Kwa jumla ujumbe wa Kenya utawajumuisha watu 161.
Kenya itashiriki katika fani 6 za michezo hio ikiwa ni Judo,Uogeleaji,Riadha,Kitwara,Raga ya wachezaji saba upande wanaume na Mpira wa Wavu wanawake.