Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Iran ambayo yalikuwa yakijibu mashambulizi ya makombora yaliyotekelezwa na Iran yanasemekana kusababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Iran mapema mwaka huu.
Jeshi la Israel IDF linasema lililenga viwanda vya makombora na maeneo mengine karibu na Tehran pamoja na upande wa magharibi wa Iran Jumamosi.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Iran inasema ina jukumu la kujitetea lakini ikaongeza kwamba Iran inatambua majukumu yake katika kuhakikisha amani na usalama katika eneo hilo.
Hatua ya Israel ya kujibu mashambulizi ya Iran yaliyohusisha makombora yapatayo 200 yaliyorushwa kuelekea Israel Oktoba 1, 2024 ilikuwa ikitarajiwa kwa muda wa wiki kadhaa.
Tehran ilisema mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh katika himaya ya Iran mwezi Julai.
Makombora mengi yalidunguliwa na Israel na wandani wake lakini mengine machache yaligonga maeneo ya kati na kusini mwa Israel.
Maafisa wa Iran walifafanua kwamba maeneo ya Tehran, Khuzestan na Ilam yaliathiriwa na mashambulizi hayo.
Jeshi lilidai kukabiliana na mashambulizi hao kwa ufanisi hata ingawa kulikuwa na madhara ya kiwango cha chini katika baadhi ya maeneo.
Kituo cha runinga kinachomilikiwa na serikali ya Iran kilipeperusha video inayoonyesha magari yakiendeshwa kama kawaida kwenye barabara za miji kadhaa huku shughuli za michezo na nyingine za shule zikiendelea kama ilivyopangwa.