Mashambulizi manne yaliyotekelezwa na kundi haramu nchini Burkin Faso yamesababisha vifo vya watu takriban 80 wakiwemo maafisa wa usalama 39 kufikia Ijumaa.
Kulingana na taarifa ,polisi wa ziada 33 waliangamia kwenye shambulizi lililotekelezwa Ijumaa katika mkoa wa Sanmatenga.
Magaidi hao pia waliangamia kwenye shambulizi hilo la kujitoa mhanga.
Nchi ya Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na msururu wa mashambulizi ya makundi ya kigaidi tangu mwaka 2015 ambapo hadi kufikia sasa watu takriban 1000 wamefariki.