Wanajeshi 21 wa Israel wauawa Gaza

Tom Mathinji
1 Min Read

Jeshi la Israel linasema wanajeshi wake 21 wameuawa huko Gaza – ikiwa ni siku mbaya zaidi kwa wanajeshi wa taifa hilo tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), Daniel Hagari, alisema inadhaniwa kuwa guruneti la roketi liligonga kifaru kimoja karibu na majengo mawili waliyokuwamo.

Alisema majengo hayo yalilipuka pengine kutokana na mabomu ya ardhini ambayo majeshi ya Israel yaliweka ili kuyabomoa.

IDF inasema bado inachunguza undani wa tukio hilo.

Israel imekuwa ikitaka kuwaangamiza Hamas tangu watu wenye silaha wawaue zaidi ya watu 1,300 katika mashambulizi ya Oktoba 7.

Takriban watu 25,295 wameuawa huko Gaza tangu jeshi la Israel lianzishe kampeni kubwa ya anga na ardhini kujibu shambulizi la Hamas, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas. Zaidi inaaminika walifariki chini ya vifusi.

TAGGED:
Share This Article