Wanafunzi 8,000 wanufaika na mradi wa elimu ya kidijitali

Tom Mathinji
1 Min Read

Wanafunzi zaidi ya 8,000 wa shule za msingi Ukanda wa Pwani wanatarajiwa kunufaika kutokana na mradi wa kitaifa wa kidijitali wa shilingi milioni 25 unaodhaminiwa na benki ya ABSA.

Benki hiyo kwa ushirikiano na Computer For Schools inaendeleza ajenda ya serikali kupitia ufadhili wa maabara ya kidijitali kwa shule za msingi na zile za upili nchini ili kuimarisha elimu ya kidijitali.

Aidha, benki ya ABSA inanuia kujenga maabara 70 yenye tarakilishi katika shule za msingi na za upili zitakazoteuliwa nchini.

Mradi huo kufikia sasa umenufaisha wanafunzi elfu 53,000 katika shule 53.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara ya kidijitali katika shule ya msingi ya Chaani eneo bunge la Changamwe, Meneja Mkurugenzi wa Benki ya ABSA Abdi Mohammed alisema mradi huo unawiana na ajenda ya uraia wa benki hiyo na akaisifia serikali kwa kuendeleza mradi wa elimu ya kidijitali nchini.

Wakati huo huo, mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi aliishukuru benki ya ABSA kwa ufadhili wake wa maabara ya tarakilishi pamoja na shilingi laki tano zitakazotumika kuwanunulia vitabu wanafunzi wa kidato cha nne.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *