Wanachama wawili wa jopo la uteuzi wa makamishna wa IEBC waapishwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanachama wawili wa jopo la kuwateua makamishna wa Tume Huru ya  Uchaguzi na Mipaka (IEBC), wameapishwa leo Ijumaa asubuhi katika Mahakama ya Upeo.

Waliokula kiapo ni Carolyne Kituku, aliyeteuliwa na Chama cha Wanasheria nchini (LSK) na Fatuma Saman aliyependekezwa na Baraza la Kidini nchini.

Uapisho wao ulifanyika katika hafla iliyoongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Wanachama saba kati ya tisa walioteuliwa na Rais William Ruto waliapishwa mapema wiki hii.

Wao ni: Lindah Gakii na Prof. Adams Oloo waliopendekezwa na Tume ya Kuwaajiri Wafanyikazi wa  Bunge, Evans Misati, Nicodemus Bore na Dkt. Koki Muli waliopendekezwa na vyama vya kisiasa, Andrew Kipkoech, aliyeteuliwa na Taasisi ya Uthibitishaji wa Mahasibu nchini ( ICPAK), na Dkt. Nelson Makanda wa Baraza la Kidini nchini.

Jopo hilo lilipewa muda wa siku 90 tangu lichapishwe katika gazeti rasmi la serikali na Rais wiki jana kukamilisha majukumu yake.

Jopo hilo litaongoza mchakato wa usaili wa Mwenyekiti  na makamishna wa IEBC  ifikiapo April 27 mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *