Maandamano ya Gen Z: Wanahabari wahimizwa kudumisha maadili

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa Mkuu Mtendaji wa MCK, David Omwoyo.

Baraza la Vyombo vya Habari hapa nchini (MCK), limetoa wito kwa wanahabari kutekeleza maadili ya hali ya juu wanaporipoti kuhusu maandamano ya Gen Z Jumatano Juni 25,2025.

Kupitia kwa taarifa, Afisa Mkuu Mtendaji wa MCK David Omwoyo, aliwataka wanahabari kuzingatia kikamilifu miongozo iliyopo ya wanahabari.

“Baraza hili linawahimiza wanahabari watakaoripoti kuhusu maandamano ya Gen ya Juni 25,2025 kudumisha utaalam wa hali ya juu, kuhakikisha taarifa zao hazikandamizi,’ alisema Omwoyo.

Omwoyo aliwataka wanahabari kuwaheshimu wenzao na umma kuhakikisha taarifa zao hazisababishi kubuniwa kwa makundi ya aina yoyote.

“Baraza hili linaheshimu uhuru wa wahariri na mtazamo wao wa kitaalam hususan katika maswala ya kitaifa kama,” aliongeza Omwoyo.

Aliwakumbusha wanahabari kuepuka kupigia debe ghasia ambazo husababisha wasiwasi katika taifa.

Website |  + posts
Share This Article