Wizara na Idara kadhaa zapewa majina mapya

Martin Mwanje
2 Min Read

Wizara mbalimbali zimepewa majina mapya katika mabadiliko ya kwanza ya Baraza la Mawaziri kuwahi kufanywa na Rais William Ruto tangu alipoingia madarakani baada ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022. 

Katika mabadiliko hayo, Ofisi ya Waziri Mwenye Mamlaka Makuu imepanuliwa na itajumuisha Wizara ya Mambo ya Nje.

Ofisi hiyo itaendelea kusimamiwa na Musalia Mudavadi.

Wizara ya Utumishi wa Umma, Jinsia na Kitendo Sawazishi imefanyiwa mabadiliko na sasa itajulikana kama Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendakazi na Usimamizi wa Utoaji Huduma.

Wizara hiyo sasa itasimamiwa na Moses Kuria.

Wizara ya Utalii, Wanyama Pori na Turathi imefanyiwa mabadiliko na sasa itajulikana kama Wizara ya Utalii na Wanyama Pori.

Wizara hiyo itaongozwa na Dkt. Alfred Mutua.

Wizara ya Masuala ya Vijana, Sanaa na Michezo imefanyiwa mabadiliko na sasa itajulikana kama Wizara ya Masuala ya Vijana na Michezo na itaendelea kusimamiwa na Ababu Namwamba.

Wizara mpya ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi iimeundwa itasimamiwa na Aisha Jumwa.

Idara ya Utendakazi na Usimamizi wa Utoaji Huduma imehamishiwa Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendakazi na Usimamizi wa Utoaji wa Huduma ambayo sasa itasimamiwa na Moses Kuria.

Idara ya Utamaduni na Turathi imepewa jina jipya na sasa itajulikana kama Idara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi na itakuwa chini ya Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi.

Aidha Idara ya Jinsia na Kitendo Sawazishi imehamishiwa Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi.

 

 

 

Website |  + posts
Share This Article