Serikali ya kaunti ya Nakuru imeapisha wanachama wa bodi za jiji la Nakuru na manispaa za Naivasha, Molo na Gilgil.
Bodi hizo zimepatiwa jukumu la uangalizi wa maendeleo katika maeneo hayo.
Hafla ya kuapisha wanachama hao ilihudhuriwa na naibu Gavana wa kaunti ya Nakuru David Kones, ambaye aliwaomba watumikie wananchi kwa njia ipasayo na watekeleze sera zitakazopitishwa na bodi zao.
Kulingana naye, bodi za miji na maeneo zitatekekeza jukumu muhimu la kusimamia masuala ya miji na maeneo na kuwa maajenti wakuu wa kutekeleza ajenda ya serikali ya maendeleo ya miji.
Kones alifichua pia kwamba serikali ya kaunti ya Nakuru inaendeleza mchakato wa kusajili na kuzindua manispaa tatu mpya ambazo ni Maai Mahiu, Njoro na Mau Narok.