Waliochukua wanao Endarasha watakiwa kutoa taarifa

Lydia Mwangi
1 Min Read

Katika tukio la moto lililotokea katika shule ya Hillside Endarasha Academy, wazazi waliochukua watoto wao baada ya mkasa huo wametakiwa kutoa taarifa kwa serikali au usimamizi wa shule ili kusaidia kutambua watoto ambao hawajulikani waliko.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Kaunti ya Nyeri, Antohny Muheria, amewahimiza wazazi waliowaficha watoto wao wawapeleke kwenye vituo vya usaidizi wa kisaikolojia kwani watoto hao walishuhudia tukio hilo la kushtua, ambalo huenda likaathiri afya yao ya kiakili siku za usoni.

Vilevile, ametoa wito kwa Wakenya wote kuungana kwa maombi na kusaidia familia zilizoathirika na mkasa huo wa moto uliotokea Alhamisi iliyopita.Haya yanajiri baada ya serikali kutangaza ni wanafunzi 17 hawajulikani waliko

Lydia Mwangi
+ posts
Share This Article