Chama cha Walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini (KUPPET), kimetishia kuitisha mgomo wa kitaifa kulalamikia huduma duni za bima ya matibabu ya SHA.
Viongozi wa KUPPET wametoa makataa ya siku saba kwa SHA kutatua changamoto zilizoko la sivyo watagoma.
Yamkini walimu wengi wamekuwa wakizuiliwa hospitalini baada ya kutibiwa kufuatia hatua ya SHA kukosa kuwalipia huduma.
Walimu walijumuishwa katika bima ya matibabu ya SHA yapata miezi mitatu iliyopita.