Walimu wa sekondari msingi yaani Junior Secondary katika kaunti ya Nandi walifanya maandamano ya amani mjini kapsabet wakisema hawatarejea shuleni hadi pale serikali itawaajiri kwa mkataba wa kudumu.
Maandamano haya yamejiri wakati ambapo shule zimefunguliwa kwa muhula wa kwanza baada ya likizo ndefu ya krisimasi .
Wakiongozwa na stephen koech lagat , milcah cherobon na wesly korir walimu hao wamesema kwamba kandarasi yao na tume ya kuajiri walimu nchini TSC ya mwaka moja iliisha Disemba 31, mwaka jana na hawako tayari kufanya makubaliano yoyote na tume hiyo kama sio ya kuajiriwa rasmi .
Walimu hao wamemtaka rais william ruto kuingilia kati kwani wanapitia changamoto si haba.
Waliongeza kusema kwamba inasikitisha kuona baadhi ya wabunge wamechukua majukumu ya tume ya kuajiri walimu nchini TSC kwa kutoa barua za uajiri kwa watu walio karibu nao.
Suala hilo kulingana nao limechangia pakubwa katika kukosa kwao kwa fursa za kuajiriwa.