Wakulima watakiwa kujisajili ili kunufaika na huduma za serikali

Martin Mwanje
1 Min Read
Serikali ya kaunti ya Makueni imeanzisha mpango wa kusajili wakulima wote kwa ushirikiano wa karibu na serikali kuu.
Hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Kilimo Kello Harsama ambaye alizuru eneo la Mbooni kukutana na wakulima.
Harsama amesema kuwa wizara ya Kilimo ikishirikiana na kaunti ya Makueni wameeka mikakati kabambe kuongeza ghala za kuhifadhi mbolea ya bei nafuu kwa ajili ya wakulima.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Makueni Lucy Mulili amewataka wakulima wajisajili kwa wingi ili kupata huduma za serikali kuu pamoja na kaunti.
Waziri wa Kkilimo katika kaunti ya Makueni Joyce Mutua ameeleza kwamba kufikia sasa, wamesajili wakulima 18,000 huku wakitarajia kusajili wakulima 160,000  kabla ya zoezi linaloendelea la kuwasajili wakulima kukamilika.
Share This Article