Wakulima wa miwa Busia wafurahia teknolojia mpya

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakulima wa miwa katika kaunti ya Busia wamekumbatia matumizi ya teknolojia mpya kunyunyiza mbolea wakati na baada ya upanzi wa miwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtambo wa unyunyizaji mbolea, wakulima wakiongozwa na Patrick Masinde walisema mtambo huo utapunguza wizi na hasara za mbolea.

Waliongeza kuwa mtambo huo wa kunyunyiza mbolea utawapunguzia madhara kwenye ngozi yanayotokana na unyunyizaji wa mbolea iliyo na kemikali kwa kutumia mikono.

Meneja Mkuu wa kampuni ya West Kenya Olepito Gerald Okoth alidokeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na hasara ya mbolea kutokana na matumizi mabaya kwa upande wa wakulima.

Teknolojia hiyo mpya itapunguza hasara hizo na kuhakikisha wakulima wanazalisha miwa kwa wingi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *