Wakulima wa chai kupokea bonasi ya shilingi bilioni 44 wiki ijayo

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakulima wa majani chai watapokea marupurupu ya mazao waliyowasilisha viwandani kufikia Juni 30 mwaka huu, kuanzia wiki ijayo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Ukuzaji Chai Nchini, KTDA, wakulima watalipwa marupurupu ya wastani ya shilingi 59 kutoka kwa malipo ya shilingi 50 kwa kila kilo moja mwaka uliopita.

Pia kiwango cha chai kilichochumwa kufikia Juni mwaka huu nchini Kenya, kilifikia kilo bilioni 1.254 ikiwa ni ongezeko kutoka kilo bilioni 1.145 kufikia mwezi Juni mwaka uliopita.

TAGGED:
Share This Article