Wakulima Ukambani watakiwa kukumbatia kilimo cha nazi

Jonathan Mutiso
1 Min Read

Wakulima katika eneo la Ukambani wametakiwa kukumbatia kilimo cha nazi kama njia mbadala ya kuongezea chakula katika eneo hilo.

Akizungumza katika uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Machakos, Lawrence Matolo ambaye ni mwenyekiti wa maonyesho hayo katika zoezi la kuwapa wakulima mbegu za nazi amewataka wakulima katika eneo la Ukambani kuzingatia kwa kina kilimo cha nazi za kisasa ambazo huchukua muda wa miaka mitano kupata mazao.

Zaidi ya mbegu 1,300 za mmea huo zimegawiwa wakulima zaidi ya mia mbili kufanya jaribio la kwanza la kuanzisha kilimo cha nazi katika eneo la Ukambani kwa jumla.

Aidha, baadhi ya wakulima wa zamani waliowahi kupanda mmea huo katika eneo hilo wameeleza kupata mazao na mapato makubwa kutokana na hali ya anga ya Ukambani japo wengi wana dhana kwamba mmea huo unaweza ukafanya vizuri katika eneo la Pwani.

Jonathan Mutiso
+ posts
TAGGED:
Share This Article