Wakili George Kithi amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Hazina ya Maendeleo ya Michezo na Sanaa (SASDF) kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kithi amerithi wadhfa huo kutoka kwa Rais wa Chama cha Riadha Kenya, Jackson Tuwei, ambaye amekuwa mwenyekiti tangu mwaka 2019.
Hafla ya kukabidhiwa mamlaka imeandaliwa Jumatano kwenye makao makuu ya Wizara ya Michezo na kushuhudiwa na Waziri Salim Mvurya.
Kithi aliteuliwa mwenyekiti wa SASDF Februari 6 na Rais William Ruto.
Hazina hiyo hujukumika na ugavi wa pesa kwa mashirikisho ya michezo, shughuli za ukuzaji talanta na hafla za kitaifa za kitamaduni.